Umuhimu wa imani
    face
  •   
  •  
Allah Mwenye kupokea toba.

Icreasefontsize decreasefontsize

Umuhimu WA ImaNi

Hakika A’amali Bora Mbele Ya Allwah Na Tukufu Zaidi Ni Imani, Kwa Hadiith Iliyo Pokewa Na Abuudhari (R.A.A.) Alipo Muuliza Mtume (S.A.W) "Ewe Mtume Wa Allwah Niipi Amali Bora? Akasema Ni Kumuamini Allwah Na Kupigania Dini Yake." (Imepokewa Na Muslim)

Nayo Ni Sababu Ya Uongofu Na Furaha Ya Dunia Na Akhera Kwaneno Lake Allwah Mtukufu. {Basi Yoyote Ambaye Mwenyezi Mungu Ataka Kumuongoza Huukundua Moyo Wake} (Al An-Am: 125)

Na Pia Imani Inamueka Mbali Muumini Na Maasi, Kasema Allwah Aliyetukuka: {Walio Muogopa Mwenyeezzi Mungu Kikiwashika Chochote Cha Shetani Hukumbuka Mara Huwa Wamekuwa Waangavu.} (Al Aaraf: 201)

Imani Ni Sharti Ya Kukubaliwa A’amali, Amesema Allwah Mtukufu {Hakika Umeletewa Wahyi Wewe Na Walio Kuja Kabla Yako Kwamba Ukimshirikisha Mwenyeezzi Mungu Itapomoka A’amali Yako Na Hakika Utakuwa Miongoni Walio Pata Hasara.} (Az-Zumar 65), Basi Imani Safi Mwenyeezzi Mungu Huibariki Na Hutakabali Kwa Imani Hiyo Dua.

   
shiriki nasi